Image
Image

EXCLUSIVE: MAFURIKO YASABABISHA MAAFA MOROGORO, WAKAZI 210 WAKOSA MAKAZI YA KUISHI.

Mafuriko Morogoro
 Na : Jimmy Mengele, Morogoro

Zaidi ya wakazi 210 mkoani Morogoro wamekosa makazi baada ya nyumba zao kusombwa na mafuriko yaliyotokana na mvua kubwa iliyonyesha mkoani humo.

Inaelezwa kuwa kutokana na mvua kubwa zinazoendelea kunyesha mkoani humo hali ya mafuriko imesababisha jumla ya kaya 57 wa wananchi wa kijiji cha Msowelo wilaya ya kilosa kuharibiwa na maji pamoja na kaya nane za wakazi wa mvuha wilaya ya morogoro kukosa makazi.

Mvua hizo ambazo zimenyesha usiku wa kuamkia April tano mwaka huu znaelezwa kusababisha mafuriko ambayo yamesomba vyakula vya wananchi pamoja na kuharibu mazao hivyo kuwafanya wawe na wasiwasi wa kukumbwa na baa la njaa.

Ng"ombe wa kiwa ndani ya maji Baada ya mvua kusababisha mafuriko.


Gari likiwa limezama Baada ya Mvua kunyesha na kusababisha mafuriko
Kutokana na maafa hayo mkuu wa wilaya ya Morogoro Mh. Saidi A manzi amewataka wananchi waishio katika mabonde kuhama ili kuepuka maafa mengine yatakayotokea siku za baadae kwani mvua bado zinaonyesha dalili za kuwepo kwa mvua kubwa.

Nyumba hizo ambazo zimeharibiwa vibaya na maji, 19 zimebomoka kabisa pamoja na miundombinu ya bara bara kuharibiwa huku madaraja yakiwa hatarini kusombwa na maji.
Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment