Hakuna tatizo kwa redio
kutopiga nyimbo ya msanii yoyote kwan redio hujiendesha yenyewe. Magic Fm
imekaa mdaa mrefu bila kupiga nyimbo za diamond na hata east Africa redio
ilikaa mdaa mrefu bila kupiga nyimbo ya ray c, amesema ruge mutahaba
Akizungumza leo
asubuhi katka kipindi cha power breakfast Mkurugenzi wa Clouds
Entertainment RugeMutahaba amezungumzia suala ambalo limekuwa gumzo katika
mitandao ya kijamii na midomoni mwa watu kuhusiana na LADY JAY DEE kutoa
kashfa nzito.
RugeMutahaba |
Ruge amesema nchi kama
nchi tunatakiwakujadili mambo ya msingi na siyo binafsi na kuwa kimya muda
mrefu kutoongelea tatizo hili kwasababu halina maslaiya taifa inatakiwa
tukae tumalize binafsi na hajui tatizo ni nini .
Clouds fm ni chombo
binafsi iliyosajiliwa na mamlaka ya mawasiliano Tanzania kwa kufuata Masharti
tofauti na kuchagua vitu vyao kuwa ni Redio ya burudani na inapanga wao nyimbo
za kupiga na sio mtu mwingine na KUSEMA WANAWEZA KUAMUA WASIPIGE
NYIMBO YEYOTE YA BONGO FLEVA.
Pia Ruge amesema kila
mtu mzuri akifanya kitu kizuri lazima kiwe na lawama na tatizo hili limeanza
vipi yeye afahamu chochote .
Amesema wana record ya
kupiga wimbo mpya wa jay dee mara 46 kwa hiyo haelewi kwanin anasema hwapigi
nyimbo zake.
Ameongeza kuwa LADY
JAY DEE anahofia band ya sky right ambayo inamilikiwa na SEBASTIAN
NDEGE ambaeni mfanyakazi wa mwandamizi wa CLOUDS MEDIA GROUP.
“Sky rights imeanza kwa
kuchukua wanamuziki toka bendi mbalimbali ikiwemo ya lady jay dee lakin sio
chanzo cha kuigopa. So jay dee anatakiwa apelike makombora yake kwa sky rights
sio kwangu” amesema Ruge
Aidha Ruge amesema
kuwa muziki ni mchezo wa kupokezana vijiti na mtu uwezi tawala sku zote kwani
sasa kuna watu wanakuja juu sana kama kina ommy dimpoz.
Kuhusu Lina na barnaba
kutopiga show amesema kuwa tatizo ni hawakupatana vizuri kwenye suala la
malipo.
Amesema kuwa clouds
media group inafanya tamashamoja kwa mwaka kwa hiyo wanaosema kuwa wanawanyonya
wasanii kwenye show wanatoa wapi ayo.
Ameongeza kuwa clouds
media group huwazamini wasanii kila week kupiga show kwenye kumbi za bilcanas
na maisha club.
LAD JAY DEE NAYE KUPITIA PAGE YAKE YA FACEBOOK KASEMA HAYAA.
LADY JAYDEE
|
0 comments:
Post a Comment