Image
Image

EXCLUSIVE: HIZI NDIO PICHA 10 ZIKIONYESHA MAJAMBAZI WALIOUAWA LEO MBEYA.

Kamanda Diwani akionyesha silaha walizokuwa wakitumia majambazi hao.
Majambazi wakiwa wamelazwa baada ya kuuawa


Kamanda Diwani akiangalia gari lililokuwa likitumiwa na Majambazi hao

Hawa ndio majambazi Waliouawa

    GARI LA MAJAMBAZI HAO


ASKARI WAKIANGALIA SILAHA ZILIZOIWEKWA MEZANI ZILIZOKUWA ZIKITUMIWA NA MAJAMBAZI HAO

HAO KAMANDA OTHMANI AKISISITIZA JAMBO BAADA YA KUWATIA NGUVUNI MAJAMBAZI HAYO.

MOJA YA SILAHA KUBWA ILIYOKUWA IKITUMIWA NA MAJAMBAZI HAO IKIWA MEZANI


Kamanda diwani akionyesha wskari wenzie moja ya jambazi lililokuwa limeshika silaha


MTANDAO wa Ujambazi nchini hususani Mkoani Mbeya umezidi kusambaratishwa  baada ya watu watano wanaodahaniwa kuwa ni majambazi kuuawa katika majibizano na Askari wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya Diwani Athumani amewaambia Wandishi wa Habari Ofisini kwake kuwa Tukio hilo limetokea leo majira ya Sita Mchana katika kijiji cha Garijembe Wilaya ya Mbeya katika Barabara ya Mbeya Tukuyu.

Alisema Jeshi la Polisi kupata taarifa za Kinterejensia waliweka mitego mbali mbali na kufanikiwa kuwanasa watu hao wakiwa kwenye gari lenye  namba za usajili T  911 BUG aina ya Toyota Spacio ambapo baada ya kusimamishwa katika eneo hilo wakitokea Kyela kuelekea Jijini Mbeya.
Alisema baada ya kusimamishwa ghafla walianza kurusha risasi ovyo  ambapo Askari walijibu mapigo na kufanikiwa kuwajeruhi wote watano ambapo waliwafikisha katika Hospitali ya Rufaa ya Mbeya kwa ajili ya Matibabu lakini Daktari alithibitisha kuwa tayari walikuwa wamekufa.
Aliongeza kuwa baada ya kufanyiwa upekuzi walikutwa na Silaha mbili ambazo ni bunduki aina ya SMG 848628 ambapo kwenye magazine zilibaki risasi 16 na bunduki nyingine aina ya Mark III yenye namba 94695J ikiwa na risasi mbili pamoja na Koa za Shaba.
Kamanda Diwani ameongeza kuwa taarifa za Kinterejensia zilieleza kuwa majambazi hayo yalijipanga kufanya uhalifu katika maeneo ya Ushirika, Tukuyu Mjini Wilayani Rungwe pamoja na Eneo la Uyole Jijini Mbeya.
Aidha alisema majina yao wala makazi yao hayakuweza kujulikana maramoja ambapo miiliehifadhiwa katika Hospitali ya Rufaa ya Mbeya na kutoa wito kwa wananchi kufika Hospitalini hapo kwa ajili ya kuwatambua ndugu zao ili wakabidhiwe kwa taratibu za mazishi.

Pia anatoa wito kwa wananchi wenye taarifa zinazohusu uhalifu kuzitoa katika mamlaka zinazohusika kwa wakati ili zifanyiwe kazi.
Picha na Mbeya yetu 



Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment