Msuguano mkali wa kumnasa kiungo nyota
mshambuliaji wa uganda, moses oloya inazidi kushika kasi na sasa simba imeamua
kufanya fitna kwa kumtumia mshambuliaji wake wa zamani, emmanuel okwi amalize
mchezo.
Simba ndiyo ilikuwa ya kwanza
kumwania oloya anayekipiga katika kikosi cha klabu ya saigon xuan thanh ya
vietnam, lakini yanga nao 'wakatia mguu'.
kwa kuwa yanga waliamua
kuingia na kuanza kazi ya kumnasa oloya likiwa ni ombi la kocha wao, ernie
brandts, aliyesisitiza anamhitaji mganda huyo, simba wameamua kumtumia okwi
ambaye pia amemsisitiza oloya kuwa sehemu sahihi ni simba.
chanzo cha uhakika kimeeleza,
simba ilimtuma geofrey nyange 'kaburu' kwenda uganda ambako alifanya mazungumzo
na oloya kwa mara nyingine akiwa katika kambi ya the cranes.
"kaburu ambaye alikwenda
kwa niaba ya (zacharia) hans pope ambaye mwanzo ndiye alizungumza na oloya. pia
alimtumia okwi amshawishi oloya kuhusiana na simba na maisha yake yalivyo,
najua atakuwa amemueleza yanga hakumfai.
"kweli okwi alifanya
naye mazungumzo na kumsisitiza kama anataka kuja tanzania, basi timu sahihi ni
simba. kwangu sidhani kama kweli oloya anaweza kubadilika maana ni rafiki wa
karibu wa okwi," kilieleza chanzo hicho cha uhakika.
"okwi na oloya
wanaelewana sana, wamekuwa marafiki kwa kipindi kirefu. hivyo dalili zote
zinaonyesha kuwa oloya atatua simba."
yanga ilifanya juhudi hadi
kumtuma mwakilishi nchini vietnam kuhakikisha inamnasa, lakini viongozi wake
walikanusha baada ya kuona mpango umejulikana na oloya aliwataka watoe dola
100,000 (zaidi ya sh milioni 160) kama alivyokuwa amewaeleza simba.
kuona hivyo, simba wakaongeza
nguvu kwa hofu ya kumkosa. timu hizo zinalazimika kusubiri mkataba wake
umalizike ili atue nchini na kila upande bado unamhitaji. taarifa zinadai nyota
huyo atatua nchini agosti 28, mwaka huu.
source: Championi.
0 comments:
Post a Comment