Image
Image

PINDA ASEMA UKUBWA UKUBWA WA WILAYA YA SONGEA UNASABABISHAKASI NDOGO YA UCHUMI KUKUA.


Saidi Makala Songea.

Waziri Mkuu Mizengo Pinda amesema ukubwa wa wilaya ya Songea Vijijini mkoani Ruvuma unafanya istahili kugawanywa na kuwa na Halmashauri mbili ya Mandaba na Halmashauri ya Songea Vijijini ili kuongeza ufanisi wa utoaji huduma kwa wananchi na kuchochea ukuaji kiuchumi. 
Mizengo Pinda - Waziri Mkuu Tanzania.
Waziri  Mkuu Pinda akiwa ziarani mkoani humo amesema ukubwa wa wilaya hiyo yenye halmashauri moja unasababisha kasi ndogo ya kukua kiuchumi  ameshauri ni vyema ikagawanywa ili watendaji wake waweze kufanya kazi kwa ufanisi zaidi.

Wakati huo huo Waziri Mkuu Pinda amewataka wakazi wa Kitongoji cha Mkenda Kivukoni ,Kijiji cha Nakawale tarafa ya Mhukuru wilaya ya Songea Vijijini waliopo  mpakani mwa Tanzania na Msumbiji kutumia vyema Soko jipya lililojengwa ili liweze kuwanufaisha katika kiuchumi.

Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment