Dk. Joyce Ndalichako
Katibu Mkuu wa Baraza la Mitihani Tanzania
(NECTA), Dk. Joyce Ndalichako amechaguliwa kuwa Rais wa Mabaraza ya
Mitihani Barani Afrika (AEAA ) kwa kipindi cha mwaka mmoja.
Ndalichako alichaguliwa kushika wadhifa huo
uliokuwa ukishikiliwa na Raia wa Kenya, aPaulo Wasanga katika mkutano
uliofanyika jijini hapa wa masuala ya elimu, ambao uliwakutanisha wadau wa
elimu kutoka nchi zaidi ya 20 za Bara la Afrika.
Baada ya kuchaguliwa, Ndalichako alisema
cheo hicho ni heshima kwa nchi ya Tanzania na Watanzania kwa ujumla na kuwaomba
wadau wa elimu kushirikiana naye kuleta mabadiliko makubwa ya elimu nchini.
Alisema katika kipindi atakachoongoza mabaraza
hayo, atahakikisha anaboresha maendeleo kwa kila nchi hususan Tanzania na
kusisitiza kuwa ushirikiano katika utendaji wa kazi ni muhimu ili kuinua sekta
ya elimu kwa nchi hizo.
Ndalichako alisema ili kufikia lengo la
ufaulu ni lazima kutoa nafasi kwa watumishi wa mabaraza ya mitihani
wajifunze mbinu za ufaulu.
Akizungumzia kuhusu mkutano huo, alisema umewezesha
wadau wa mabaraza ya mitihani kutoka bara hilo kutathimini usahihishaji
wa mitihani na kuweza kutumia kompyuta kwa ajili ya kuchagua majibu
sahihi ya mitihani.
Ndalichako aliiomba serikali kushirikiana naye
ili kuwezesha sekta ya elimu kukua.
Nipashe.

.jpg)
0 comments:
Post a Comment