Salum mkambala, Dar es Salaam
Mahakama ya
Hakimu Mkazi Kisutu, Dar es Salaam
imewahukumu pasipo shaka,miaka mitatu jela au kulipa adhabu ya shilingi
milioni 21kila mmoja viongozi wanne wa kampuni ya Kusimamia na Kuendesha Upatu
(DECI) na kumuachia huru mshtakiwa wa tano baada ya washtakiwa hao wanne
kupatikana na hatia katika mashtaka yote mawili ya kuendesha shughuli hizo
kinyume cha sheria.
Washtakiwa
hao ni Jackson Mtares, Dominic Kigendi, Samuel Mtares, Timotheo ole Loitingye
na mshtkaiwa wa tano aliachiwa huru baada ya ushahidi katika shauri hilo
kutomtia hatiani pasipo shaka ni Arbogast Francis Kipilimba ambapo jumla ya
mashahidi 16 wa upande wa mashtaka walitoa ushahidi wao.
Katika
mashataka yao walidaiwa kuendesha na kusimamia shughuli za upatu kinyume na
sheria na kukusanya amana kutoka kwa umma bila ya kuwa na leseni ambapo
wanadaiwa kutenda makosa hayo kati ya mwaka 2007 na Machi 2009 katika Makao
Makuu ya DECI, Mabibo, Dar es Salaam.
Akitoa hukumu
mbele ya hakimu mkazi wa mahakama hiyo Aloyce Katemana katika shtaka la kwanza
amewataka washtakiwa hao kutumikia kifungo cha miaka mitatu jela au kulipa
faini ya sh.milioni tatu kila mmoja na katika shtaka la pili amewahukumu kila
mmoja kutumikia kifungo cha miaka mitatu jela au kulipa faini ya sh.milioni 18
kila mmoja huku ikitoa amri na maelekezo kwa serikali kupitia benki kuu,BOT
kwamba,akaunti tano zilizokuwa na
takribani bilion i,16,viwanja ,nyumba na magari viuzwe na fedha zirudishwe kwa
wanachama wa DECI.


0 comments:
Post a Comment