Dar es Salaam.
Kundi la
wanaharakati wa kulinda wanyama pori wamekamilisha matembezi ya kilomita 650
kutoka Arusha kwenda mjini Dar es Salaam.
Wanaharakati hao
waliandaa matembezi hayo kulalamikia visa vya uwindaji haramu wa ndovu na
vifaru.
Matembezi hayo kwa
jina "Walk for the Elephant" yalidhaminiwa na shirika la African
Wildlife Trust (AWT) na yalilenga kuhamasisha watu kuhusu athari za uwindaji
haramu barani afrika.
Naibu waziri wa
mali asili na utalii wa Tanzania Lazaro Nyalandu anasema ndovu 30, 000
waliuwawa kwa ajili ya pembe zao barani Afrika mwaka jana na nchini Tanzania
pekee kila siku ndovu 30 huuwawa.



0 comments:
Post a Comment