Wenye mabasi madogo ya abiria nchini Rwanda
wamelalamikia sheria mpya inayowataka kupitia katika maeneo fulani kwenye mji
mkuu Kigali.
Wanasema kwamba mamlaka ya mji wa Kigali iliwabagua na
kutoa leseni za barabara ambazo hazina wateja .
Mamlaka ya mji ilitoa leseni za barabara muhimu kwa
wenye mabasi makubwa na hivyo wale wenye magari madogo sasa wamesalia bila
biashara.
Shirikisho la usafiri wa umma, kampuni ya basi ya
Kigali (KBS) na kapmuni nyingine ya Royal express pekee ndizo zilipewa tenda ya
miaka mitano ya kusafirisha watu katika maeneo maalum mjini humo.


0 comments:
Post a Comment