Image
Image

MRADI WA TANZANIA WATEULIWA NA - WEF



Jukwaa la Kimataifa la Uchumi- WEF,  limeteua mradi wa ukanda wa uchukuzi wa kati mpaka upande wa Magharibi unaopakana na nchi jirani, kama mradi wa mfano wa kuwekewa msukumo wa kifedha na kiteknolojia katika utekelezaji wake, ili uwe mfano wa ushiriki wa sekta binafs katika ujenzi wa miundo mbinu barani Afrika.

Mradi huo utahusisha ujenzi wa Barabara, Reli na kuiboresha Bandari ya Dar es salaam kwa manufaa ya mataifa ya Tanzania, na nchi jirani za upande wa magharibi na kaskazini magharibi.

Katika Mkutano wa WEF uliofanyika DAVOS nchini Uswisi, kuanzia januari 22 hadi 26 mwaka huu, kati ya miradi 51 ya bara la Afrika, mradi huo ambao kwa asilimia tisini upo nchini Tanzania, ulichaguliwa kusaidiwa kifedha na kiutendaji ili kuukamilisha, ambapo wiki ya kwanza ya mwezi April viongozi wa Umoja wa Afrika wanatarajia kukutana nchini kwa lengo la kuweka mipango ya kuufanikisha.

Waziri wa Uchukuzi, Dk Harrison Mwakyembe, ambaye alikuwa miongoni  mwa ujumbe wa Tanzania ulioongozwa na rais Kikwete kwenye mkutano huo, ameelezea serikali inakusudia kuunda kamati yenye wajumbe wanane kwa lengo la kusaidia kufanikisha mpango huo.




Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment