Image
Image

NSSF YATOA MSAADA WA KUCHANGIA ELIMU YA SEKONDARI LINDI.


 Wanafunzi mkoani lindi wakiwa darasani, huku wakikabiliwa na uhaba wa walimu wa masomo ya sayansi,(Picha na Maktaba yetu).

Abdulaziz Ahmed- lindi.
=================
Wito umetolewa kwa Serikali Nchini kutoa upendeleo wa Vifaa katika sekondari za Kata ikiwemo upendeleo wa kupatiwa walimu wa kutosha wa masomo ya Sayansi ili kusaidia Ukuaji wa Uchumi kwa wakazi wa Mikoa ya kusini ili waufaike na fursa zilizopo kiuchumi.

Hayo yamebainishwa katika Taarifa ya Wanafunzi wa Shule ya Sekondari ya Kineng'ene iliyopo katika Halmashauri ya Manispaa ya Lindi, katika hafla fupi ya kupokea Meza 2 za maabara zilizotolewa na Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF) zenye  thamani zaidi ya Sh.11.99 milioni.

Taarifa hiyo iliyosomwa na Mwalimu Esther Lumato imebainisha baadhi ya changamoto zinazoikabili shule hiyo ikiwemo ukosefu wa umeme, hatua inayozorotesha ufanisi katika masomo.

Naye, meneja wa Mfuko wa NSSF mkoani Lindi, Bi Shani Mtani amewataka wanafunzi kutokubali kudanganywa kwa vishawishi vyovyote badala yake wazingatie masomo hususani ya Sayansi, kwani ndiyo yatakayowasaidia katika maisha yao ya baadae.

Awali akitoa taarifa ya Elimu katika manispaa hiyo, Kaimu Afisa elimu sekondari, Maurus Ndunguru alisema utoro bado ni changamoto kubwa Mkoani Lindi na kwamba kwa wanafunzi waliochaguliwa kujiunga na kidato cha kwanza mwaka huu kati ya wanafunzi 767 walioripoti hadi sasa ni wanafunzi 229 ikiwa sawa na 29.9%.
Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment