Image
Image

UBALOZI WA CHINA WATOA MSAADA WA KIBINADAMU KWA WAADHIRIKA WA MAFURIKO MKOANI MOROGORO JIJINI DAR ES SALAAM


 Mkuu wa kitengo cha Maafa,ofisi ya Waziri Mkuu, Luteni Jenerali mstaafu, Sylvester Chacha Rioba akipokea msaada wa vitu mbali mbali kwa , Balozi wa China hapa nchini, Lu Youqing jijini Dar es salaam.


Ubalozi wa China hapa nchini umetoa msaada wa kibinadamu wa vitu mbalimbali ikiwemo vyakula, magodoro, mablanketi, nguo, mafuta wenye thamani ya shilingi milioni 30, kwa ajili ya waathirika wa mafuriko wilayani Mvomero mkoani Mororogo.

Akikabidhi msaada huo jijini Dar es salaam, kwa mkuu wa kitengo cha Maafa, Ofisi ya Waziri Mkuu, Luteni Jenerali mstaafu, Sylvester Chacha Rioba, Balozi wa China hapa nchini, Lu Youqing amesema Tanzania na China zina udugu wa kihistoria na kuongeza kwamba maafa yaliyotokea Morogoro yamewagusa wananchi wa China kwa kiasi kikubwa.
Amesema ana imani katika uongozi madhubuti wa Rais Jakaya Kikwete, wananchi wa Morogoro waliokumbwa na mafuriko watavuka vyema katika kipindi hiki kigumu na kujenga upya maisha yao.

January 22 mwaka huu, mvua kubwa zisizotabirika kutokea milima ya Kilosa na Mvomero mkoani Morogoro zilizasababisha mafuriko makubwa katika mto Mkundi, hali iliyosababisha kukatika kwa daraja la Dumila ambalo linaunganisha barabara kuu ya Dodoma na Morogoro.

Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment