Image
Image

KIWANDA CHA KUTENGENEZEA MAGODORO CHATEKETEA KWA MOTO,NA KUSABABISHA HASARA YA MAMILIONI YA SHILINGI,MWANZA.




Moto mkubwa umeteketeza sehemu ya kiwanda cha kutengeneza magodoro kilichoko eneo la mkuyuni jijini mwanza na kusababisha hasara ya mamilioni ya shilingi, huku ajira za wafanyakazi zaidi ya 100 wa kiwanda hicho zikiwa katika hatihati ya kusimama kwa muda usiojulikana.

Moto ulioteketeza kiwanda hicho cha vitanda manufacturing company limited, kinachomilikiwa na kundi la makampuni ya hashamjamal, ulianza majira ya saa 1.30 usiku na kufanikiwa kuzimwa saa 6  kwa msaada wa vikosi vya uokoaji na zimamaoto vya halmashauri ya jiji la mwanza na uwanja wa ndege wa mwanza, ambapo baadhi ya mali yakiwemo magogoro, majengo, mitambo pamoja na magari yaliungua huku baadhi ya nyaraka zikiteketea na kubaki majivu.

Uongozi wa kiwanda hicho kupitia kwa afisa masoko jayesh joshi umesema chanzo cha moto huo ni hitilafu ya umeme huku ukishindwa kueleza thamani ya mali yote iliyoteketea. 

Baadhi ya watu walioshuhudia tukio hilo ambalo ni la pili kutokea katika kiwanda hicho cha magodoro ya comfy, baada ya tukio la kwanza lililotokea mwezi oktoba mwaka 2006 wanaeleza mazingira yaliyopelekea kiwanda hicho kuungua.
Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment