Image
Image

Wachimbaji wa ndani na nje ya Tanga wakaidi agizo la Serikali la kuwataka kusitisha zoezi la uchimbaji eneo la kigongoi.




Wachimbaji zaidi ya 200 kutoka maeneo tofauti ya ndani na nje ya mkoa wa tanga ambao wanaodai kuwa wamepewa vibali vya uchimbaji na wizara ya nishati na madini wamegomea agizo la serikali la kuwataka kuacha uchimbaji katika eneo la mgodi wa kata ya kigongoi kwa sababu wanalipa kodi kwa serikali.

Akizungumza katika mkutano wa dharura wa kujadili agizo la serikali uliofanyika katika mgodi huo,mwenyekiti wa chama cha ushirika cha wachimbaji madini kata ya kigongoi Augustino Hassan amesema hawataondoka katika eneno hilo hadi serikali itakapokwenda kufanya tathmini ya uhalali wa kuchimba madini katika mgodi huo kwa kushirikiana na wadau wa wizara ya nishati na madini pamoja na idara ya misitu na nyuki mkoa wa tanga.

Baadhi ya wachimbaji wadogo waliokutwa katika mgodi huo wamesema kitendo cha kuagizwa kuacha kuchimba madini kihalali hakina lengo zuri kwa sababu makundi ya vijana wanaofuata sheria yakizuiwa kuacha kufanya kazi hiyo yatakwenda kujikita katika vitendo viovu vya uporaji katika jamii hatua ambayo ni ukiukwaji wa sheria za nchi.

ufuatia hatua hiyo mkuu wa wilaya ya mkinga Bi. Mboni Mgaza amesema hatua hiyo ya kufunga mgodi huo imekuja kutokana na uharibifu wa mazingira unaofanywa katika mgodi huo sanjari na kufanya ukaguzi wa wachimbaji wenye leseni ili utaratibu mpya uweze kufanywa kisheria kwa lengo la kuepuka vitendo vya uharibifu wa vyanzo vya maji yanayotumika na wakazi wa tarafa ya maramba.

Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment