Image
Image

Wanajeshi 54 nchini Nigeria Wahukumiwa Kifo.





Mahakama ya Jeshi la Nigeria imewahukumu adhabu ya kifo wanajeshi 54, kwa kugoma kupambana na wapiganaji wa Kiislam wa kundi la Boko Haram.
Wanajeshi hao ambao wametiwa hatiani kwa kukaidi amri ya jeshi, wanatuhumiwa kukataa kusaidia kukomboa miji mitatu iliyotekwa na Boko Haram mwezi Agosti.
Mwanasheria wa wanajeshi hao 54, amesema wanakabiliwa na adhabu ya kuuwawa kwa kupigwa risasi.Wanajeshi wengine watano walikutwa hawana hatia.
Kundi hilo la wanajeshi limelalamika kuwa walikuwa hawajapewa silaha za kutosha na risasi ili kupigana na Boko Haram.
Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment