Image
Image

BAN KI-MOON apongeza makubaliano ya mahasimu wa wili wa Sudan Kusin kukubaliana kusitisha mapigano,licha ya kutokukubaliana katika mgawanyo wa madaraka


Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Bwana  BAN KI-MOON  amepongeza makubaliano ya hivi karibuni ya kusitisha mapigano kati ya pande mbili zinazohasimiana Sudan Kusini.
Hata hivyo Katibu Mkuu huyo wa Umoja wa Mataifa ameonesha kusikitishwa kwake na pande hizo mbili kutokubaliana namna ya mgawanyo wa madaraka.
Msemaji wa Bwana  BAN amewaambia Waandishi wa Habari kuwa hakutapatikana amani Sudan Kusini  iwapo  Rais  SALVA KIIR   na kiongozi wa waasi, Bwana    RIEK MACHAR   hawataweka mbele maslahi ya raia.
Msemaji huyo Bwana    STEPHANE DUJARRIC  amesema Umoja wa Mataifa hauna taarifa za mapigano mapya tangu pande hizo zinazopingana Sudan Kusini kutiliana saini juzi.
Serikali ya Sudan Kusini na waasi zimekubaliana kukamilisha makubaliano ya kukomesha mgogoro wa nchi hiyo uliodumu kwa mwaka mmoja sasa itakapofika  tarehe tano mwezi ujao.

Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment