Image
Image

Breaking News: Rais kikwete afanya mabadiliko ya wakuu wa mikoa

Rais kikwete amefanya mabadiliko ya wakuu wa wilaya na kuteua wakuu wapya na wengine kutenguliwa nafasi zao.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete leo, amefanya uteuzi wa wakuu wapya wa Wilaya, kuwahamisha vituo vya kazi huku wengine wakiachwa.
Habari zilizotufikia hivi punde zinasema majina 27 mapya yameteuliwa huku wengine 11 wakitupwa nje ya uongozi huo.
Walio teuliwa ni pamoja na Katibu Mkuu wa Zamani wa TFF, Freddrick Mwakalebela, Mtangazaji wa TBC,
Shaban Kisu, Katibu wa Hamasa wa Jumuiya ya Umoja wa Vijana wa CCM (UVCCM), Paul Makonda, Makamu Mwenyekiti wa UVCCM Taifa, Mboni Mhita na aliyewahi kuwa RPC, Zolothe Steven.

Majina hayo yametangazwa na Waziri Mkuu, Mizengo Pinda mjini Dodoma mchana huu.

Waziri mkuu pia akataja majina ya wakuu wa wilaya 12 ambao uteuzi wao umetenguliwa na rais kutokana na sababu mbalimbali ikiwemo umri na matatizo ya kiafya ambapo miongoni mwa majina mashuhuri ni pamoja aliyekuwa mkuu wa wilaya ya kiteto martha umbula, james ole millya longido na elibariki emmanuel kingu aliyekuwa mkuu wa wilaya ya igunga.
Mhe waziri mkuu amebainisha kuwa mabadiliko hayo yanaanza kazi mara moja huku wakuu wapya 27 wakipatiwa semina maalum ya uongozi na namna ya kutekeleza majukumu yao itakayotolewa na ofisi ya waziri mkuu tawala za mikoa na serikali za mitaa.
Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment