Image
Image

CHAD latangaza kuwauwa BOKO HARAM 270

Jeshi la CHAD limetangaza kuwauwa wanamgambo MIA MBILI NA SABA wa kundi la BOKO HARAM katika mpaka wa nchi hiyo na Cameroon.
Taarifa ya jeshi la CHAD imesema wanamgambo hao wameuliwa kufuatia mapigano karibu na mji wa GARAMBU uliopo katika mpaka wa nchi hiyo na CAMEROON.
Mwanajeshi mmoja wa CHAD ameuliwa na wengine Tisa kujeruhiwa katika mapigano hayo.
Aidha Jeshi la CHAD, limefanikiwa kuchukua silaha na magari mawili ya Boko Haram yaliyoachwa na wapiganaji hao waliokimbia baada ya kuzidiwa nguvu.
Hivi karibuni nchi jirani na NIGERIA ziliunda kikosi maalumu cha kupambana na wanamgambo wa Boko Haram baada ya kushuhudia mashambulio ya wanamgambo hao na kuhatarisha usalama wa raia.
Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment