Image
Image

Hali si shwari Nigeria zikiwa zimesalia wiki mbili kufanya uchaguzi mapigano yanashika kasi


Mapigano yanaendelea katika maeneo mbalimbali nchini Nigeria zikisalia wiki mbili za uchaguzi wa urais.

Mashambulizi yaliendelea kushuhudiwa Jumapili Februari 1 katika miji ya Gombe Potiskum, kasazini mshariki mwa Nigeria, huku mapigano yakiendelea pia kati ya kundi la Boko Haram na majeshi ya Chad na Nigeria katika miji ya Gamboru na Maiduguri, mashariki mwa nchi.

Mashambulizi hayo katika miji ya Gamboru na Maiduguri yanasadikiwa kutekelezwa na kundi la Boko Haram, wakati zikisalia wiki mbili ili uchaguzi wa rais ufanyike.

Wanamgambo wa Boko Haram walianzisha mashambulizi katika mji wa Maiduguri, ambao ni ngome yao kuu ya zamani, huku raia wengi wakionwekana katika mji huo baada ya kuyahama makazi yao kufuatia mapigano yaliyokua yakijiri katika maeneo walipokua wakiishi.

Kwa mujibu wa mashahidi, wanamgambo wa Boko Haram, ni wengi kaskazini mwa mji wa Maiduguri, na imekua ni vigumu kwa jeshi la serikali kukabiliana na wanamgambo hao. Wakati huo huo, helikopta za jeshi la Chad ziliendesha Jumapili Februari 1 mashambulizi ya angani katika ngome za kundi la Boko Haramkatika mji wa Gamboru. Miji ya Potiskum na Gombe ilishambuliwa kwa siku hio.

Hayo yakijiri mashambulizi ya kujitoa muhanga yalishambuliwa katika miji ya Potiskum na Gombe. Watu 7 wameuawa na wengine 7 wamejeruhiwa katika mashambulizi ya kujitoa muhanga katika miji ya Potiskum na Gombe katika jimbo la Yobe. Kwa mujibu wa shahidi, mtu aliye jitoa muhanga alijilipua akiwa ndani ya basi mbele ya nyumba ya Sabo garbu, mfuasi wa chama tawala, akiwa pia mgombea katika uchaguzi wa Wabunge utakaofanyika Februari 17

Inasadikiwa kuwa wanajeshi 2500 wa Chad wamewasili nchini Cameroon, kwa mujibu wa chanzo cha kijeshi, huku wanajeshi wengine wakiwa walitumwa kando ya mto el-Beïd, wakiwa na silaha nzitonzito, kama vifaru, na bunduki zingine za kivita.
Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment