Image
Image

Hali ya kiafya ya mama mzazi wa mtoto mwenye ulemavu aliyetekwa na kufariki dunia baada ya kukatwa viungo ni mbaya


Hali ya ESTHER JONAS, ambaye ni mama mzazi wa mtoto mwenye ulemavu wa ngozi aliyetekwa na kufariki Dunia baada ya kukatwa viungo, imeelezwa na madaktari wa hospitali ya rufaa BUGANDO alikolazwa kuwa ni mbaya baada ya kushindwa kupumua kutokana na kuvimba sehemu kubwa ya mwili ikiwamo kichwani.

ESTER JONAS, mwenye umri wa miaka 30 ambaye jana amefanyiwa upasuaji wa kichwa katika hospitali ya rufaa ya BUGANDO imebadilika ghafla usiku wa kuamkia leo na madaktari wamemuwekea mipira puani kwa ajili ya kumsaidia kupumua ili kuokoa maisha yake.

Mkuu wa kitengo cha dharura katika hospitali ya BUGANDO DK. DERICK DAVID amesema kuwa hali ya mama huyo sio nzuri na kwamba kwa sasa anapumua kwa shida na pia hazungumzi na kuongeza kuwa kinachofanyika sasa ni kuendelea kumsafisha vidonda na kumpa antibaotiki ya kukausha vidonda.Kwa kutaka kufahamu zaidi Bofya hapa>>>http://www.itv.co.tz/new.
Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment