Image
Image

Haya ndio mambo ya msingi aliyo yazungumza Daz Baba juu ya kutumia Dawa za kulevya.


                              Na.Msaka Noti Manoti - Dar es Salaam
Mwanamuziki wa bongo fleva nchini Tanzania Daz  baba au Dazi mwalimu amesema kuwa ameshangazwa na uvumi ambao ulisambaa kwamba yeye ni mgonjwa na na anaomba msaada jambo ambalo amesema sio kweli.

“Mwenyewe ni meshangaa taarifa hizo mimi nipo na wanangu tumechili tuna sikia taarifa hizo sasa hata sielewi pengine labda kuna mbaya wangu ambaye alitaka kuniharibia.

Mapema leo April 5/2015 amefunguka kupitia moja ya Show ya XXL Clouds Fm wakati alipokuwa  akifanyiwa Interview juu ya sanaa na mwenendo wa muziki akiwa kama mwanamuziki wa Kitambo sana huku waki Review ngoma zake kadhaa ambazo zimefanya poa tokea time.

Daz baba anasema kuwa watu walishtuka mno kuona picha ile haswa mashabiki wangu kwakuwa mimi ni rasta siwezi kutumia madawa nikachoka kiasi hicho mpaka kuomba msaada na wala situmii dawa za kulevya.

“Niseme tu kwamba stori hizi ni uzushi mtupu kwani picha walio piga ni washkaji wa Morogoro na walifanya hivyo kwa nia na madhumuni ya kuniharibia na inaonyesha wametumwa ili kuharibu maisha yangu ya saana ya Muziki cha msingi mashanbiki wangu wayapuuze tu hayana ukweli”amesema Daz .

Dj Fety.Nikitu gani watu wanakuwa wanasema wewe unavuta unga na wewe unasema huvuti?.

“Mimi sivuti unga ila kinachopelekea hivyo ni namna ninavyo jichanganya  na watu tofauti ila sijawahi kuvuta bangi mimi ni Rasta far"Daz Baba.

B12 imekuharibia vipi kwa jamii?

“Ni kweli ina haribu sana na haipendezi kwa hilo bangi na vuta ila kama Dawa mi Ras siunajua sijawahi kutumia hata kidogo unakuta labda nimekunywa nime sizewabaya wangu wanapiga picha wanatuma ili wanafaike kwa mgongo wangu”Daz Baba.

Daz ameendelea kufunguka na kusema kuwa analaani kwanza kutumia Dawa za kulevya kwakuwa pia anaishi kwa misingi ya familia yake na watanzania kama ikiwa ni kioo kinacho mmulika,ambapo katika nyimbo zake wimbo wake wa usihukumu kauzungumzia vizuri ila watu wana mhukumu kuwa anatumia Dawa,amesema maisha anayoishi hapendi kujikweza anaishi maisha ya kawaida sawa na wengine.




Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment