Image
Image

JAPAN YATOA MSAADA WA SHILINGI MILIONI 165 KWA AJILI YA MASHINE YA KUKAMULIA MAFUTA YA ALIZETI, CHATO MKOANI GEITA

Waziri wa Ujenzi Dkt. John Pombe Magufuli ambaye pia ni Mbunge wa Chato (katikati) akifurahia jambo wakati akizungumza Balozi wa Japan Masaki Okada (kulia), pamoja na wawakilishi kutoka Hospitali ya Taifa Muhimbili baada ya sherehe ya utiaji sahihi wa mkataba wa uwekwaji mashine ya kukamualia mafuta ya Alizeti wilayani Chato. Hafla hiyo ya utiaji saini umefanyika leo jijini Dar es Salaam.
Balozi wa Japan, Masaki Okada, akifafanua jambo kwa Waziri wa Ujenzi ambaye ni Mbunge wa jimbo la Chato Mhe. John Magufuli kabla ya tukio la utiaji sahihi nyumbani kwake jijini Dar es Salaam.
Balozi wa Japan Masaki Okada akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) kuhusiana na mradi wa uwekwaji wa mashine ya kukamulia mafuta ya alizeti wilayani Chato ambao utagharimu shilingi Milioni 165 na kuwa na uwezo wa kuzalisha Lita 1,600 na magunia 80 ya alizeti kwa saa.


Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Chato Clement Berege akitoa pongezi kwa Balozi wa Japan Masaki Okada (hayupo pichani) mara baada ya utiaji saini wa mkataba wa mradi wa uwekwaji wa mashine ya kukamulia mafuta ya Alizeti wilayani Chato.
Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Chato Clement Berege pamoja na Balozi wa Japan Masaki Okada wakiweka saini ya msaada wa fedha kwa ajili ya mradi wa uwekwaji mashine ya kukamulia mafuta ya Alizeti, Chato. Huku Waziri wa Ujenzi ambaye pia ni Mbunge wa Chato Mhe. John Magufuli akishuhudia tukio hilo.
Waziri wa Ujenzi Dkt. John Magufuli akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) katika tukio hilo.
Balozi wa Japan nchini, Masaki Okada (wa pili kulia) akiwa na Waziri wa Ujenzi Dkt. John Magufuli ambaye pia ni Mbunge wa Chato (wa pili kushoto) katika picha ya pamoja na wa wawakilishi kutoka Wilaya ya Chato mara baada ya hafla ya utiaji saini kwa ajili ya msaada wa mashine ya mafuta ya kukamulia alizeti wilayani humo.
Mkuu wa Wilaya ya Chato, Rodrick Mpogolo, akitoa salamu za shukrani kwa Balozi wa Japan Masaki Okada (hayupo pichani) mara baada ya tukio hilo jijini Dar es Salaam.


Waziri wa Ujenzi Mheshimiwa Dkt. John Magufuli (Mb) (kulia) akimpongeza Balozi wa Japan Masaki Okada (kushoto) mara baada ya zoezi la utiaji sahihi kati ya Serikali ya Japan na Uongozi wa Wilaya ya Chato kukamilika.
Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment