Serikali ya Tanzania na washirika wake wa kimaendeleo wamesaini makubaliano mapya yenye lengo la kuongeza juhudi za kumaliza ukeketaji na ndoa za utotoni nchini humo.
Baada ya kusainiwa kwa makubaliano hayo, Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto wa Tanzania Bibi Sophia Simba amesema serikali imedhamiria kutokomeza kabisa vitendo hivyo ili wasichana waweze kufurahia maisha yao bila ya kuwa na majuto katika maisha yao yote. Amesisitiza kuwa Tanzania itahakikisha kuwa hakutakuwa na wasichana watakaoolewa wakiwa na umri wa chini ya miaka 18, hususan baada ya katiba iliyopendekezwa kupitishwa. Tanzania ni moja ya nchi zenye kiwango kikubwa sana cha ndoa za utotoni duniani, karibu wasichana wawili kati ya watano wanaolewa kabla ya kufikia umri wa miaka 18.
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
0 comments:
Post a Comment