Image
Image

Kenya yapendekeza kuhimiza biashara ya ndani ili kuzuia bidhaa za viwango vya chini kuingia Afrika mashariki

Rais Uhuru Kenyatta wa Kenya ametoa wito kwa Jumuiya ya Afrika mashariki kuhimiza biashara ya ndani ili kupunguza bidhaa zenye viwango vya chini kuingia katika kanda hiyo.
Akizungumza mjini Nairobi baada ya kukutana na maofisa wa shirikisho la vyama vya wajasiriamali wa sekta isiyo rasmi la Afrika mashariki, Rais Kenyatta amesema bidhaa za eneo hilo zinaweza kuifanya kanda hiyo kuwa eneo la kuzalisha bidhaa badala la kuagiza kutoka nje. Amesema inasikitisha kuona kanda hiyo inatunmia pesa nyingi kuagiza bidhaa zinazotengenezwa kwa malighafi wanayosafirisha nje.
Amesema serikali yake imeweka mipango ya kuwawezesha vijana na makundi mengine kwa ajili ya kuboresha maisha yao. Maofisa wa jumuiya ya wajasiriamali wamependekeza kuwekwa kwa maduka katika sehemu ambazo wakazi wa nchi wanachama wanaweza kuonyesha na kuuza bidhaa zao kwa urahisi.
Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment