Image
Image

Mahakama ya Kenya yabatilisha vifungu vya sheria

Mahakama Kuu ya Kenya imetupilia mbali baadhi ya vifungu vya sheria mpya ya kupambana na ugaidi kikiwemo cha kuvibana vyombo vya habari.
Mahakama hiyo imekitoa kifungu kinachoruhusu kuvichukulia hatua na kuviadhibu vyombo vya habari endapo vitachapisha habari zinazoelezewa “kuwa na uwezekano wa kusababisha hofu au hali ya hatari”. 
Uamuzi huo uliotangazwa na Mahakama ya Katiba ya Kenya hapo jana umechukuliwa kuwa pigo kwa Rais Uhuru Kenyatta ambaye amekuwa akikabiliwa na mashinikizo ya kumtaka aimarishe usalama wa nchi baada ya mlolongo wa mashambulio kadhaa yaliyofanywa ndani ya ardhi ya nchi hiyo likiwemo la mwaka 2013 katika majengo ya maduka ya Westgate jijini Nairobi lililosababisha vifo vya watu 67.
 Muungano wa upinzani na makundi ya kutetea haki za binadamu yamepinga sheria mpya ya usalama iliyopitishwa mwezi Disemba mwaka jana yakisema kuwa inakandamiza uhuru wa msingi wa raia. 
Licha ya kutupilia mbali baadhi ya vifungu vya sheria hiyo jopo la majaji watano wa Mahakama ya Katiba limebakisha kama vilivyo vifungu vingine vingi vya sheria hiyo kikiwemo kile kinachoruhusu watuhumiwa kushikiliwa kwa muda wa siku 360 badala ya siku 90 bila kufikishwa mahakamani na kile kinachowataka wenye nyumba kutoa taarifa za wapangaji wao. 
Mwangi Njoroge, wakili wa Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali amesema serikali inafikiria kukata rufani ya kupinga uamuzi huo
Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment