Mjumbe w a Halmashauri Kuu ya Taifa ya Chama Cha Mapinduzi kupitia wilaya ya Lindi Mjini ,Mama SALMA KIKWETE ameitaka jamii ku paza sauti zao kuwasemea watoto wenye mahitaji maalum .Amesema watoto hao wanakabiliwa na matatizo mbalimbali na hawana mtu wa kumw eleza matatizo yao.Mama SALMA KIKWETE ambaye ni Mke wa Rais JAKAYA MRISHO KIKWETE a metoa rai hiyo alipotembelea kitengo cha wanafunzi wenye mahitaji maalum katika Shule ya Msingi Mpilipili ,Wilaya ya Lindi Mjini .Ame sema watoto wenye mahitaji maalum wanakabiliwa na matatizo mengi ikilinganishwa na watoto wengine na pia matatizo yao hayafanani hivyo ni jukumu la kila mtu katika jamii kuw asaidia watoto hao ili wa ishi kama watoto wengine.Akisoma taarifa ya kitengo cha wanafunzi wenye mahitaji maalum mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi Mpilipili , Bwana FADHILI MTITIMA ame sema kitengo hicho kilianzishwa mwaka 1993 kikiwa na wanafunzi watano na hivi sasa kuna wanafunzi 20 .
Home
News
Mama Salma Kikwete aitaka jamii kupaza sauti zao ili watoto wenye mahitaji maalum kuweza kusaidiwa
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
0 comments:
Post a Comment