Siku nne baada ya kuungua kwa nyumba iliyosababisha vifo vya
watu sita wa familia moja, Dar es Salaam, moto mwingine umeteketeza
sehemu ya juu ya jengo la ghorofa mbili la Shirika la Nyumba la Taifa
(NHC) lililopo katikati ya jiji.Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam,
Kamishna Suleiman Kova, alisema hakuna mtu aliyefariki wala kujeruhiwa
katika tukio hilo lililotokea kwenye makutano ya Mitaa ya Libya na
Mosque, Wilaya ya Ilala.Kamanda Kova alisema Polisi walipata taarifa jana
saa 5.30 asubuhi kuwa kunguru ndio walisababisha hitilafu ya umeme na
jengo hilo kushika moto na kutekekeza mali ambazo thamani yake
haijafahamika.Alisema moto huo ulioanza taratibu na kuongezeka ghafla kutokana na mitungi ya gesi iliyokuwamo kwenye jengo hilo.
Meneja wa NHC Mkoa wa Dar es Salaam, Jackson Maagi
alisema jengo hilo lilikuwa na familia zaidi ya 10 na kwamba shirika
hilo litahakikisha kuwa waathirika wanapatiwa nyumba za kuishi wakati
utaratibu mwingine ukiendelea kufanyika. “Tungekuwa sisi ni chanzo cha tukio hilo tungesema
tuwafidie lakini kwa kuwa sisi siyo chanzo, tutawapa nyumba kwa ajili
ya kujihifadhi, labda pengine chanzo halisi kitakapopatikana ndipo
tutajua tufanye nini,” alisema Maagi.Hata hivyo, mmoja wa wakazi katika jengo hilo,
Ahlim Abdullah alisema jengo hilo lilikuwa na familia nne katika ghorofa
ya kwanza na ofisi kadhaa katika ghorofa ya pili iliyoteketea kwa moto.
Akizungumzia chanzo cha moto huo, alisema:
“Waliokuwa nje wanasema walimwona kunguru akisababisha shoti na moto
kuanza kusambaa.”
Kamanda wa Kikosi cha Zimamoto na Uokoaji, Kanda
Maalumu ya Dar es Salaam, Jeswald Nkongo alisema baada ya kupewa taarifa
kuwa kuna moto, walituma gari la kwanza kwa ajili ya kufanya tathmini
ya ukubwa wa moto ndipo walipobaini kuwa ulikuwa mkubwa na tayari
ulikuwa umeshaanza kusambaa.
Wananchi walalamika
Baadhi ya wananchi waliofika mapema katika eneo
hilo walikitupia lawama Kikosi cha Zimamoto kwa kufika mapema lakini
kilichelewa kuanza kuuzima moto kwa sababu ambazo hazikufahamika.
“Jengo limeanza kuungua limekuja gari likiwa na
maji kidogo, wamekaa muda mrefu hawajui wafanye nini hadi tulipoanza
kusaidia kuwatoa watu waliokuwa ndani.
This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
0 comments:
Post a Comment