Image
Image

Mbio za Marathoni kuanza Machi Mosi mkoani Kilimanjaro Moshi Kaskazini mwa Tanzania

Shirikisho la Riadha duniani IAAF na Chama Cha kimataifa cha mbio ndefu na fupi za marathon AIMS wamepima na kupitisha njia zitakazotumika kwa ajili ya mbio za kimataifa za Kilimanjaro Marathon zitakazofanyika March 1 mkoani Kilimanjaro Moshi Kaskazini mwa Tanzania. 
Mbio hizo zinashirikisha wakimbiaji mahiri kutoka nchi mbalimbali ikiwemo Kenya, moja ya nchi maarufu katika mchezo wa riadha Afrika na Dunia kwa ujumla. Kukiwa hakuna mabadiliko makubwa ya njia zilizotumika mwaka jana, washiriki watapita Barabara ya Mweka huku wakipata fursa ya kuuona Mlima Kilimanjaro, ambao ndio mrefu kuliko yote Barani Afrika, ikiwa kama sehemu ya kukuza utalii wa ndani pia. 
Mbio zitaanza Chuo Cha Ushirika mapema saa 12.30 asubuhi, huku kukiwa na mbio za full Marathon, half marathon kwa wakimbiaji wa kawaida, half Marathon tena kwa watu wenye ulemavu na Kilometa 5 kwa ajili ya afya.
Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment