Image
Image

Meli yenye uwezo mkubwa wa kubeba kontaina 1040 yawasili mtwara na kuvuta mamia kuishuhudia



Mtwara:Meli kubwa
Meli kubwa kabisa inayojulikana kwa jina la HAMMONIA PHAFICUM  yenye urefu wa mita 209 na uwezo wa kubeba kontaina 1040 toka nchini Singapole imewasili katika bandari ya mtwara na kuwa vuta wakazi wengi kuja kuiona na kusema kuwa ikitunzwa vizuri italeta neema kwa watanzania.

Meli hiyo ambayo ni ndefu  imevunja rekodi  ya meli ndefu ambayo ilishawahi kufika bandarini hapo yapata miaka minne iliyopita ambayo ilikuwa na urefu wa mita 205.

Wakazi wa mtwara wamesema kuwa meli hiyo ili iweze kudumu wanaiomba serikali kuipatia vifaa vya kisasa ili iweze kuendelea kutoa huduma mjini humo na ikiwa ni meli ambayo nikubwa wao wanajionea fahari kuwa na chombo kikubwa kama hicho na hivyo kuwasihi watanzania wenzao kuwa na umoja na kukilinda na kukipenda chombo chao hicho.

Bandari ya mtwara ilijengwa miaka ya 1940 na imeonyesha ukomavu wa hali ya juu na kuonekana kuwa ni imara baada ya kuhimili kishindo cha Meli hiyo kubwa kutua bandarini hapo.


Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment