Image
Image

Museveni:Taifa la Iran lina nia thabiti kwa nchi za Afrika


Rais Yoweri Kaguta Museveni wa Uganda amesema kuwa, Jamhuri ya Kiislamu ya Iran daima imekuwa ikionyesha kuwa ni taifa lenye nia njema, rafiki na mshirika makini kwa nchi za Kiafrika.
Rais Museveni ameyasema hayo mjini Kampala wakati alipokutana na kufanya mazungumzo na Dakta Muhammad Javad Zarif, Waziri wa Mambo ya Nchi za Nje wa Iran na kusisitiza kwamba, Uganda inakaribisha juhudi za kustawisha mashirikiano na Jamhuri ya Kiislamu ya Iran katika nyanja zote za kisiasa, kiuchumi, kiutamaduni, kielimu na kiusalama. Rais Museveni amesifu maendeleo makubwa ya Iran katika nyanja mbalimbali, na ameeleza hamu ya serikali ya Kampala ya kustafidi na uzoefu wa Iran katika masuala ya sayansi na teknolojia. Rais wa Uganda ameisifu nafasi muhimu ya Iran katika kusaidia kuimarisha amani na utulivu katika eneo la Mashariki ya Kati na kueleza matumaini yake kwamba mwenendo wa mazungumzo ya nyuklia kati ya Iran na kundi la 5+1 utakuwa na matokeo chanya kwa Iran.
Kwa upande wake Dakta Zarif ameeleza kuwa, Uganda ni nchi inayopiga hatua kubwa kimaendeleo na kusisitiza kwamba Iran ina azma kubwa ya kufungua ukurasa mpya wa ushirikiano kati ya nchi hizo mbili. Waziri wa Mambo ya Nch za Nje wa Iran amesema kuwa, vitendo vya kigaidi, ukandamizaji na vitendo vya kufurutu mipaka ni miongoni mwa changamoto kubwa zinazoyakabili maeneo mengi ulimwenguni, kutokea Mashariki ya Kati, Afrika na Ulaya na kusisitiza kwamba kuimarishwa ushirikiano kutasaidia kutokomeza vitisho vya makundi hayo.
Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment