Image
Image

Niger kutuma majeshi Nigeria kupambana na Boko Haram

Bunge la Niger limeidhinisha kwa kauli moja mpango wa kupelekwa wanajeshi wa nchi hiyo nchini Nigeria kwa lengo la kushiriki kwenye kikosi cha nchi za eneo la Magharibi mwa Afrika kitakachopambana na kundi la kigaidi la Boko Haram.Taarifa zinasema kuwa, serikali ya Niger itatuma wanajeshi wake 750 nchini Nigeria kwa lengo la kupambana na magaidi wa Boko Haram. Nchi za Chad, Cameroon, Niger na Nigeria zimetangaza kuunda kikosi cha pamoja cha askari 8,700 cha kukabiliana na kundi hilo. Kwa upande mwingine wanamgambo wa Boko Haram wamewateka nyara 20 waliokuwa ndani ya basi la abiria huko kaskazini mwa Cameroon na kisha kuwauwa 12 miongoni mwao.
Hadi sasa serikali ya Cameroon haijathibitisha au kukanusha taarifa hiyo ya kutekwa nyara na kuuawa raia wa nchi hiyo. Tokea mwaka 2009, kundi la Boko Haram licha ya kufanya vitendo vya utekaji nyara watu hasa wasichana na wanawake, limekuwa likifanya mauaji na jinai mbalimbali dhidi ya wananchi wa kaskazini mwa Nigeria na nchi zinazopakana na nchi hiyo.
Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment