Image
Image

Wagonjwa wa saratani hucheleweshwa hospitali'

ZAIDI ya asilimia 80 ya wagonjwa wa saratani hufikishwa Hospitali ya Rufaa ya Bugando wakiwa kwenye hatua ya mwisho ya ugonjwa ambayo husababisha kutopata matibabu ya kinifu.Hali hiyo imebainishwa na Mkurugenzi Mkuu wa hospitali hiyo, Kien Mteta kwenye maadhimisho ya siku ya saratani duniani iliyoadhimishwa Bugando kwa Kanda ya Ziwa."Wagonjwa wengi wanaoletwa hospitalini hapa wanakuwa tayari saratani imeshaenea na kuharibu maeneo muhimu kwenye miili yao, hali hiyo inatufanya tushindwe kukosa tiba mbadala," alisema.Mteta aliongeza pia ufinyu wa uelewa kwa jamii dhidi ya saratani imekuwa kikwazo kikubwa cha watu kuchelewa kufika hospitali kutokana na kutokujua dalili za mwanzoni za saratani.Akizungumza na waandishi wa habari Mteta alisema, takwimu zilizopo Hospitali ya Taifa ya Saratani Ocean Road iliyopo jijini Dar-Es-Salaam zinaonesha kuwa asilimia 60 ya wagonjwa wanaotibiwa hospitalini hapo wanatokea Kanda ya Ziwa.Kwa kuona tatizo hilo na kupunguza msongamano huo uliopo Ocean Road serikali ikishirikiana na wadau kutoka nchini mbalimbali imejenga Kitengo cha Tiba ya mionzi chenye thamani ya dola za Kimarekani 7,000,000.Jengo hilo limejengwa kwa kuzingatia viwango vya kimataifa vya IAEA na kuidhinishwa na TAEC lenye vyumba mbalimbali kwa ajili ya kutolea huduma hiyo."Tayari tumeshapokea mashine moja ya Liner Accelerator, msaada kutoka Italy kwa ajili ya tiba ya mionzi ambayo inatarajiwa kufungwa na kuanza kazi hivi karibuni hospitalini hapa," alisema.Akitaja dalili kuu sita za ugonjwa wa saratani, Mkuu wa Idara ya Kitengo cha Saratani, Nestory Masalu alisema, ”kupungua uzito kwa kiwango kikubwa,kutoka kwa majimaji sehemu zisizo za kawaida,kidonda kisichopona,mabadiliko ya tabia, uvimbe usio na maumivu; hizo ni dalili kuu za saratani zote duniani," alisema.Alisema, dalili hizo ni viashiria vikubwa kwa mtu mwenye saratani ambapo jamii inatakiwa kuelewa pindi watakapoona dalili hizo wawahi haraka hospitali kwa ajili ya vipimo ili kubaini tatizo mapema.

Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment