Image
Image

Pellegrini awapa Yaya Toure na Wilfried Bony unyunyu wa kusherehekea ushindi wa Afcon

Kocha Manuel Pellegrini amesema Yaya Toure na Wilfried Bony hawatacheza dhidi ya Stoke City kwenye Ligi Kuu England kesho Jumatano licha ya kwamba watakuwa wamemaliza majukumu yao kwenye michuano ya Afcon 2015 walipokuwa na kikosi chao cha Ivory Coast. 
Mastaa hao juzi Jumapili walicheza fainali ya Kombe la Mataifa ya Afrika dhidi ya Ghana mjini Malabo, Guinea ya Ikweta, lakini kocha wao klabuni Manchester City alisema hawatarudi na kucheza katika mechi ya Ligi Kuu itakayofanyika katikati ya wiki hii. 
Pellegrini alisema pia hana wasiwasi juu ya hali ya usalama kwa nyota wake hao walishiriki fainali za Afcon nchini Guinea ya Ikweta, ambako juzi ilielezwa usalama uliimarishwa zaidi ili kuepuka kilichotokea kwenye mechi ya nusu fainali kati ya Ghana na wenyeji hao ambapo mashabiki walifanya fujo zilizosababisha mechi kusimama kwa karibu dakika 30.
Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment