Mwanariadha Oscar Pistorius ambaye anatumikia kifungo baada ya Mahakama
ya Afrika Kusini kumkuta na hatia ya mauaji ya aliyekuwa mpenzi wake,
Reeva Steenkamp kwa kumpiga risasi ndani ya nyumba yake sasa
amepandishwa hadhi gerezani.
Kwa mujibu wa utaratibu wa Magereza ya
Afrika Kusini wafungwa wanapangwa kwa madaraja tofauti, Pistorious
alikuwa 'Daraja B' lakini kwa sasa yuko 'Daraja A', ambapo hapa alipo
sasa anaruhusiwa kukutana na wageni wowote wanaomtembelea mbali na
ilivyokuwa mara ya kwanza alipotakiwa akutane na ndugu zake tu.
Kwa sasa
anaweza pia kusikiliza Radio, kuvaa vitu vya thamani kama cheni na
pete. Msemaji wa familia yake Annalise Burgess amesema mwanariadha huyo
kwa sasa amepandishwa hadhi na kuwa 'Daraja A', anaweza kupiga simu na
kununua vyakula anavyotaka.
Hata hivyo suala la Oscar kupandishwa daraja
limewakera wafungwa wenzie walioko gereza la Death Island, ambao
wamelalamika kuwa mwanariadha huyo anapewa hadhi hiyo ndani ya kipindi
cha muda mfupi wakati wao wamekaa muda mrefu gerezani na hawajapata
hadhi hiyo.
Pistorius alihukumiwa kifungo cha miaka mitano jela mwaka
jana mwezi August.
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
0 comments:
Post a Comment