Image
Image

Rais KIKWETE afanya uteuzi wa tume ya Utumishi wa umma na Tume ya Usuluhishi na Uamuzi

Rais JAKAYA KIKWETE, amefanya uteuzi wa Wenyeviti wa Tume ya Utumishi wa Umma na Tume ya Usuluhishi na Uamuzi -CMA.
Katika uteuzi huo, Rais KIWETE amemteua Jaji mstaafu STEPHEN BWANA kuwa Mwenyekiti wa Tume ya Utumishi wa Umma na EDRISSA MAVURA, kuwa Mwenyekiti wa Tume ya Usuluhishi na Uamuzi –CMA.
Sambamba na uteuzi huu, pia Rais amewateua Makamishna katika Tume hizo.
Makamishna wateule wa Tume ya Utumishi wa Umma ni GEORGE YAMBESI, Alhaji MBILA, MWALIMU ALLY, ADIEU NYONDO, SALOME MOLLEL na EVELYNE INATISA.
Makamishna wateule wa Tume ya Usuluhishi na Uamuzi-CMA ni PAUL KINEMELA, MATHIAS KABUNDUGURU, NJAA KIBWANA, JONES MAJURA, JAFFARI OMARI na SUZANE NDOMBA.
Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment