Image
Image

Serikali imekiri kuwepo kwa changamoto katika mchakato wa uandikishaji wa Daftari la wapigakura Mipakani

   

Dodoma Bungeni
Serikali imekiri uwepo wa changamoto katika uandikishaji wa daftari la wapiga kura hususani katika maeneo ya mipakani mwa nchi ili kuhakikisha kuwa ni watanzania pekee ndio wanaoandikishwa.waziri mkuu mh mizengo pinda ameyasema hayo bungeni mjini dodoma wakati akijibu swali la Mh.Josephine Gezabuke  aliyetaka kufahamu utaratibu utakaotumiwa na serikali kupitia tume ya uchaguzi kuhakikisha watu wasio raia wa tanzania hawaandikishwi katika daftari hilo katika zoezi linaloendelea.Ameongeza kuwa njia rahisi ya kuwaondo wasio raia hapa nchini ni kupitia operesheni kadhaa lakini zoezi hilo halizai matunda kutokana na kuingizwa raia kutokana na mwingiliano mkubwa uliopo miongoni mwa raia na wasio raia katika maeneo ya mipakani.Hata hivyo ameiagiza idara ya uhamiaji kufanya shughuli hiyo kwa utaratibu wa kisheria na kwamba serikali italisimamia zoezi hilo kikamilifu ili kutenganisha makundi ya raia na wasio raia japo kuna changamoto kubwa ya namna ya kuwatambua raia na wasio raia kutokana na mwingiliano mkubwa uliopo.


Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment