Serikali ya Kenya imetangaza kupanua mpango wake wa kuboresha makazi
duni katika miji mingine ikiwa ni sehemu ya kuwawezesha vijana kote
nchini humo.
Msemaji wa ikulu Manoha Esipisu amesema, tangu mpango huo uanze
Septemba mwaka jana, sehemu kubwa ya mtaa wa Kibera pamoja na makazi
mengine mjini Nairobi zimesafishwa na barabara mpya kujengwa. Amesema
kumekuwa na ongezeko la biashara kwa wafanya biashara wadogo na vijana
wamefanikiwa kupata ajira.
Akizindua mpango huo mwaka jana, rais Uhuru Kenyatta wa Kenya
alisema miradi hiyo itaboresha mitaa duni ikiwemo Mukuru kwa Njenga,
Korogosho na Mathare katika kaunti ya Nairobi. Ameongeza kuwa mpango huo
unalenga kuwafanya wakazi wa maeneo hayo waishi katika mazingira safi
yatakayowaepusha na vitendo vya uhalifu.
0 comments:
Post a Comment