Image
Image

Sheikh Khalifa:Aitaka serikali kuweka utaratibu wa huliheshimu vazi la Hijab Kenya



Katibu Mtendaji wa Baraza la Maimamu na Wahubiri nchini Kenya "CIPK" ameitaka serikali kuweka mikakati ya kuhakikisha vazi la hijab ya Kiislamu linaheshimiwa kwa mujibu wa katiba ya nchi hiyo.
 Sheikh Mohamed Khalifa ameongeza kuwa, sharti la hijab ni kusitiri sehemu zote za mwili wa mwanamke, na wala isimuonyeshe sehemu zake za mwili, na kusababisha matamanio kwa wanaume. 
Sheikh Khalifa aliyasema hayo katika siku ya kimataifa ya kuadhimisha vazi la hijab, inayofanyika tarehe Mosi Februari kila mwaka na kusisitiza kwamba, serikali ya Nairobi inapasa kuweka mikakati kabambe ili kuhakikisha vazi hilo linapewa heshima ipasayo kwa mujibu wa katiba ya nchi hiyo. Katibu Mtendaji wa CIPK ameongeza kuwa, vazi la hijab ni ishara ya stara, faragha na ucha Mungu kwa mwanamke wa Kiislamu. Hata hivyo, vazi hilo la stara ya mwanamke wa Kiislamu linakabiliwa na chamgamoto kadhaa ulimwenguni na hasa mashuleni, vyuoni, makazini na hata kwenye sehemu za umma. Sheikh Khalifa amesema kuwa, changamoto wanayokumbana nayo wanawake wa Kiislamu ni taasisi za binafsi zinazohujumu haki zao, kauli iliyoungwa mkono na viongozi wengine wa dini ya Kiislamu nchini Kenya.   
Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment