Kundi la kigaidi la Boko Haram limetishia kuwa litavuruga uchaguzi mkuu
wa Nigeria utakaofanyika mwezi ujao wa Machi.
Abubakar Shekau, kiongozi
wa kundi la Boko Haram nchini Ngeria ametoa vitisho kwamba kundi hilo
litavuruga uchaguzi mkuu wa nchi hiyo.
Akizungumza kupitia mkanda wa
video uliorushwa jana Shekau amesema kuwa Boko Haram haitaruhusu
kufanyika uchaguzi mkuu huko Nigeria hata kama kundi hilo litalazimika
kupoteza roho za wananchama wake.
Uchaguzi mkuu wa Nigeria umepangwa
kufanyika tarehe 28 mwezi ujao wa Machi. Uchaguzi mkuu nchini Nigeria
awali ulipangwa kufanyika Februari 14, lakini uliakhirishwa kwa wiki
sita nyingine kwa sababu za kiusalama, khususan kutokana na kushtadi
mashambulizi ya Boko Haram kaskazini mashariki mwa nchi hiyo.
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
0 comments:
Post a Comment