Image
Image

Tanesco haiwezi kuto walipa wateja waliopata majanga ya moto – Serikali

Serikali imesema Shirika la Umeme nchini (Tanesco) haliwezi kuwalipa fidia wananchi waliopatwa na majanga ya moto yaliyosababishwa na hitilafu ya umeme, kwani ni kuliongezea mzigo.

Hayo yalisema na Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Pereira Silima, wakati akizungumza na NIPASHE juu ya kuwapo kwa sheria ya fidia kwa wananchi waliopatwa na majanga ya moto yaliyosababishwa na hitilafu ya umeme.

Silima alisema suala la Tanesco kulipa fidia kwa wananchi waliopatwa na majanga ya moto yaliyosababishwa na hitilafu ya umeme ni jambo gumu ambalo haliwezi kutekelezwa kwa haraka. 
Alisema Tanesco ina majukumu mengi ikiwamo la kuhakikisha wananchi wanapatiwa umeme, hivyo kuliongezea mzigo mwingine ni kutaka kulifilisi.

Aliongeza kuwa mbali na kutokea kwa majanga ya moto mara kwa mara yanayosababishwa na hitilafu ya umeme, siyo kweli kwamba Tanesco limehusika moja kwa moja kusababisha majanga hayo.

Alisema sikuh izi kuna watu wanajiunganishia umeme kiholela kwa kuwatumia watu wa mitaani kuwaunganishia umeme jambo ambalo linasababisha hitilafu ya umeme na wakati mwingine kusababisha majanga.

Silima alisema kuwa mbali na wananchi kujiunganishia umeme kiholela, pia wananchi wengi wananunua vifaa vya umeme ambavyo siyo imara kutokana na kutothibitishwa na Shiria la Viwango Tanzania (TBS).

“Ki ukweli kuhusu Tanesco kuanza kulipa fidia kwa wananchi waliofikwa na majangwa ya moto kulikosababishwa na hitilafu ya umeme ni vigumu, kwa sababu hitilafu ya umeme inaweza kusababishwa na vitu vingi,” alisema Silima.

Alisema kama wananchi wanataka kuwapo kwa sheria hiyo, ni lazima wadau mabalimbali wakae vikao na kujadili kabla haijapelekwa bungeni kama muswada na baadaye kuwa sheria.

Silima alisema katika nchi nyingine sheria iyo ipo, kwa mashirika yao ya umeme kuwalipa wateja wake ikigundulika kuwa uzembe wa shirika la umeme umesababisha kuungua kwa nyumba.

Hivi karibuni, kumekuwapo na matukio mbalimbali ya nyumba kuungua kunakosababishwa na hitilafu ya umeme, likiwamo tukio la watu sita wa familia moja kuteketea kwa moto katika ajali ya moto iliyotokea  Kipunguni jijini Dar es Salaam.
Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment