Image
Image

Tanzania na Burundi zalaumiwa kuhusu hali ya DRC


Umoja wa Mataifa umezituhumu serikali za Tanzania na Burundi kuhusiana na hali katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo. Ripoti mpya ya kundi la wataalamu wa umoja huo kuhusu Kongo, imeituhumu Tanzania kuwa imewaruhusu viongozi wa kundi la waasi wa FDLR kuandaa mikutano nchini humo. Imeeleza pia kwamba wanajeshi wa Burundi wametekeleza unyanyasaji wa kingono.Taarifa hiyo ya Umoja wa Mataifa imebainisha kuwa tangu mwaka wa 2013, viongozi wa FDLR na baadhi ya washirika wao wa kisiasa kutoka Ulaya wamekuwa wakikutana nchini Tanzania.
Hata hivyo serikali ya Tanzania imekanusha kabisa madai hayo ilipoulizwa na wachunguzi wa Umoja wa Mataifa ikisema kuwa, haijawahi kukaribisha mikutano yoyote ya waasi ndani ya ardhi yake na kwamba majeshi yake hayajawahi kuwa na mazungumzo yoyote na wapiganaji wa FDLR. Umoja wa Mataifa umesema pia kuwa, una ushahidi wa pesa zilizotumwa kutoka taifa hilo la Afrika Mashariki kwa baadhi ya washukiwa nchini Jamhuri ya kidemokrasia ya Kongo. Ripoti hiyo pia imelaumu kundi hilo la FDLR kwa kutotekeleza ahadi yake ya kukabidhi silaha na kujisalimisha kufikia Januari mwaka huu.


Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment