Image
Image

UNICEF:Lishe Duni kwa watoto ni sababu inayochangia changamoto kubwa za kiafya kwa watoto DRC

Mfuko wa Watoto Umoja wa Mataifa (UNICEF) umetangaza kuwa, lishe duni inayowakabili watoto katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo ni moja kati ya changamoto kubwa zaidi za kiafya ziinazoikabili nchi hiyo.
Mwakilishi wa UNICEF nchini Kongo Pascal Villeneuve amesema kuwa, taasisi hiyo ya kimataifa inalipatia kipaumbele suala la kupambana na lishe duni nchini Kongo, na kuongeza kuwa, serikali ya Kinshasa na taasisi nyingine nchini humo zinapaswa kuelewa kwamba licha ya kupiga hatua muhimu katika baadhi ya sekta za kimaendeleo, lakini nchi hiyo bado haijapiga hatua zozote za kimsingi katika suala la kutokomeza lishe duni kwa watoto. Pascal Villeneuve ameongeza kuwa, lishe duni imesababisha asilimia arobaini na tatu ya watoto wa Kongo kukabiliwa na matatizo ya ukuaji na kuwa na uelewa mdogo wakati wa kuanza shule. Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo licha ya kuwa na maliasili na utajiri mkubwa wa madini, lakini inahesabiwa kuwa moja kati ya nchi masikini duniani. Idadi kubwa ya wananchi wa nchi hiyo wanaishi chini ya mstari wa umasikini
Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment