Image
Image

Vijana waliomaliza mafunzo ya JKT watakiwa kujiajiri wenyewe kulingana na mafunzo waliyo yapata na sio kuandamana



Vijana waliohitimu mafunzo ya Jeshi la Kujenga Taifa -JKT-  wametakiwa kujiari katika shughuli mbalimbali kulingana na mafunzo waliyoyapata wakati wakisubiri ajira zao na sio kufanya maandamano jambo ambalo ni kinyume na sheria za jeshi.
Kauli hiyo imetolewa na baadhi ya wazee wa Mkoa wa Ruvuma waliopokuwa wakizungumzia kwa nyakati tofati,  taarifa za baadhi ya vijana waliohitimu Mafunzo ya Jeshi la Kujenga Taifa kutangaza kufanya maandamano ya siku tatu mfululizo usiku na mchana jijini Dar es Salaam ili kushinikiza kuonana na Rais JAKAYA KIKWETE kumweleza matatizo ya ajira wanayokabiliana nayo.
Wamesema katika mafunzo hayo vijana wanaandaliwa kujiajiri na kubuni mbinu halali za kuijitengezea kulingana na mafunzo waliyoyapata ambayo sio mafunzo ya kutumia sialaha tu peke yeke.
Naye  mmoja wa wastaafu wa Jeshi la Wananchi Tanzania, Bwana  SEBASTIAN NYONI amesema mafunzo  ya Jeshi la Kujenga Taifa hayakuanzishwa kwa ajili ya kuwapatia ajira vijana wanahotimu bali kuwaandaa kwa ajili ya kulijenga taifa kwa namna mbali mbali ikiwa ni pamoja na ujasiriamali.

Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment