Image
Image

Wachezaji wa Manchester United wachunguzwa kwa kutengenza mkanda wa ngono

Wachezaji kadhaa wa klabu ya Manchester United wanafanyiwa uchunguzi baada ya kuhusishwa na tukio la kutengeneza mkanda wa ngono lililofanyika ndani ya ukumbi wa starehe wa usiku.
Mwanamke mmoja ambaye hajatajwa amerekodiwa akiwa anafanya vitendo vinavyoshabihiana na ngono huku akiwa na mmoja kati ya wachezaji wa Manchester United ambaye si raia wa England kwenye choo cha klabu ya usiku huku moja kati ya wachezaji wenzie akiwa anarekodi tukio hilo akiwa juu ya mlango. 
 Mwanamke aliyehusika kwenye tukio hilo alihojiwa na gazeti moja la kila siku huko England ambako alielezea jinsi alivyofedheheshwa na tukio hilo na kusema tangu wakati huo amekuwa akilia na hakutaka kueleza zaidi juu ya kilichotokea. Mwanamke huyo ana hofu ya kuwa wachezaji wengine wa kikosi cha United wanamfahamu na wataonyeshana video inayoonyesha kitendo hicho ambacho kitamshushia heshima. 
Klabu ya United haijatoa taarifa rasmi juu ya tukio hili na hadi sasa hakuna mchezaji aliyetajwa kuhusishwa na tukio hilo.
Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment