Image
Image

Wakazi wa mateka walalamikia ubovu wa bara bara Manispaa ya Songea

Wakazi wa eneo la Mateka pamoja  na Waendesha Bodaboda katika Manispaa ya Songea Mkoani Ruvuma wamelalamikia ubovu wa barabara ya Songea Girls hadi Mateka  kwamba  haipitiki wakati wa mvua  na kusababisha  ajali  za mara kwa mara kutokana na ubovu.
Wamelalamikia ubovu wa barabara hiyo na kusema  kero hiyo inashindwa kutatuliwa   na sasa wamechoka na ahadi za kila siku za kuitengeneza barabara hiyo.
Wakazi hao wamewaomba viongozi wao kutowasahau kwa kuwa nao ni wakazi wa Manispaa ya Songea.
Kwa upande wake Diwani wa Kata ya Mateka, Manispaa ya Songea Bi. MARISTELA  MAPUNDA amesema barabara hiyo iko katika mpango wa matengenezo ya  kawaida.

Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment