Image
Image

Wanamgambo 20 wa al Shabab wauawa

AbdulQader Muhammad Mkuu wa Wilaya ya Lower Shabelle nchini Somalia amesema kuwa, kwa akali wanamgambo 20 wa al Shabab wameuawa kwenye shambulio lililofanywa na ndege za kivita karibu na mji wa Marga kusini mwa Somalia. Abdulqader Muhammad ameongeza kuwa, shambulio hilo lililofanywa na ndege ya kigeni kwenye kambi ya al Shabab, limeharibu magari na boti kadhaa za wanamgambo hao.
Wakati huohuo, kundi la kigaidi la al Shabab nchini Somalia limetekeleza shambulio dhidi ya uwanja wa ndege wa Mogadishu na kuwauwa wafanyakazi wanne na kuwajeruhi wengine kadhaa. Polisi ya Mogadishu imeeleza kuwa, watekelezaji wa shambulio hilo wakiwa garini walilifyatulia risasi kadhaa kundi la wafanyakazi waliokuwamo uwanjani hapo. Taarifa iliyotolewa na Polisi ya Mogadishu inaeleza kuwa, msaidizi wa mkuu wa uwanja wa ndege wa Mogadishu ni miongoni mwa watu waliouawa kwenye shambulio hilo.
Mwaka 2011, majeshi ya Somalia yakisaidiwa na Kikosi cha Kulinda Amani cha Umoja wa Afrika nchini Somalia AMISOM yalifanikiwa kuwafurusha wanamgambo wa al Shabab kutoka mji mkuu wa nchi hiyo. Kundi la al Shabab licha ya kutekeleza operesheni mbalimbali za kigaidi ndani ya Somalia, limekuwa likitekeleza operesheni kadhaa nje ya nchi hiyo na hasa nchini Kenya.
Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment