Image
Image

Wapiganaji 40 wa kundi la IS nchini Libya wauawa katika mashambulizi ya anga yaliyofanywa na Misri

Wapiganaji 40 wa kundi la IS nchini Libya wameuawa katika mashambulizi ya anga yaliyofanywa na Misri.
Mashambulizi hayo yalifanywa dhidi ya ngome za kundi hilo zilizoko nchini Libya siku moja baada ya kundi hilo kutoa video inayoonyesha wakiwachinja raia 21 wa Misri ambao ni wakristo wa dhehebu la Coptic nchini Libya.
Taarifa iliyotolewa na jeshi la Misri imesema, mashambulizi hayo yaliyolenga kambi za mazoezi pamoja na maghala ya silaha ya kundi hilo, yalifanywa kwa kulipiza kisasi vitendo vya kigaidi ndani na nje ya Misri.
Hii ni mara ya kwanza kwa Misri kuthibitisha hadharani kuwa inafanya mashambulizi ya anga dhidi ya kundi hilo lililo nchi jirani ya Libya.
Wakati huohuo jeshi la anga la Libya pia limesema kuwa limefanya mashambulizi ya anga katika kambi moja ya kundi la IS mjini Darna, mashariki mwa nchi hiyo.
Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment