Image
Image

Breaking News:Mvua kubwa iliyoambatana na upepo mkali yaua 35 na kujeruhi 55kata ya mwakata wilaya ya kahama Mkoani shinyanga


Mvua ya mawe iliyokuwa imeambatana na upepo mkali imesababisha maafa ambapo watu 35 wamefariki huku 55 wakijeruhiwa kutokana na kuangukiwa na nyumba zao kutokana na mvua hiyo kuambatana na upepo mkali Wilayani kahama mkoani shinyanga.

Mkuu wa wilaya ya kahama Benson Mpesya amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na yupo katika eneo la tukio kusimamia zoezi la kuokoa majeruhi na kufukua miili ya marehemu.

Hata hivyo kwa upande mwingine Kamanda wa polisi mkoani Shinyanga Justus Kamugisha akizungumza kwa njia ya simu amethibitisha kutokea kwa vifo hivyo ambapo amesema kuwa  watu waliofariki dunia kutokana na mafuriko hayo wameangukiwa na nyumba na miti hadi kupoteza maisha ambapo amesema hadi sasa wamethibitisha watu 38 wamepoteza maisha huku 55 wakiwa majeruhi.
Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment