Image
Image

Hali mbaya ya hewa yakwamisha oparesheni ya kutafuta miili 150 ya watu waliokufa kwenye ndege ya Ujerumani


Hali mbaya ya hewa imekuwa kikwazo cha kukwamisha oparesheni ya kutafuta miili ya watu waliokufa ,   kwenye   ndege ya Ujerumani iliyoanguka Ufaransa na kuua watu wote 150 waliokuwa ndani yake.

Polisi wa Ufaransa wamesema hali mbaya ya hewa ya milima ya Alps ilipoanguka ndege hiyo ,  huenda ikasababisha ichukue siku kadha kuipata miili hiyo.

Wachunguzi wanasema mahali ilipoanguka ndege hiyo panaogopesha mno na Waziri wa Mambo ya Nchi za Nje wa Ujerumani ,  amezungumzia picha za kutisha za ajali hiyo.

Ndege hiyo aina ya Airbus A  320 ilitokea Barcelona, Hispan ia ikiwa ina kwenda  Duesseldorf, Ujerumani  ,  na miongoni mwa abiria walikuwemo Wajerumani 60 na raia 45 wa Hispania ambayo imetangaza siku tatu za maombolezo.

Wakati huo huo ,   Wizara ya Mambo ya Ndani ya Ufaransa imetangaza kupatikana kwa kisanduku cha ndege hiyo chenye vifaa vinavyorekodi mawasiliano na matukio ya ndege inapokuwa angani .

Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment