Amesema
kuwa Maiti zimehifadhiwa katika
hospitali ya wilaya ya Mufindi mkoani iringa pamoja na baadhi ya majeruhi ambapo majeruhi wawili
ambao hali zao ni mbaya sana wamepelekwa katika hospitali ya rufaa ya iringa
kwa mujibu wa mashuhuda wa ajali hiyo.
Wanasema kuwa chanzo cha ajali ni mwendo kasi
wa basi hilo ambapo walimweleza Dereva Kupunguza mwendo lakini hakuweza kuelewa
na hivyo katika mwendo kasi aliokuwa nao ndipo wakakutana na lori hilo na hatimaye
kuvaana uso kwa uso baada ya juhudi za kulikwepa lori kufeli kutokana na
barabara hiyo kuwa na mashimo yaliyoweza kufanya gari hilo kushindwa kukwepa
mashimo hayo na hivyo kutokea kwa ajali.
Hata
hivyo katika ajali hiyo imeelezwa kuwa wakati wakuwaokoa majeruhi na kutoa
maiti wamekuta madaftari ya wanafunzi wa Chuo kikuu cha Dar es Salaam ambapo
inaelezwa kuwa katika gari hilo wanafunzi hao walikuwa ni wengi lakini bado
haijafahamika kwamba walikodi gari hilo la Majinja ama la,lakini katika
hospitali ya mufundi ndugu na jamaa wapo hospitalini hapo kwaajili yakuangalia
ndugu zao na kutambua miili ya waliofariki dunia kufuatia ajali hiyo.
0 comments:
Post a Comment